Malalamiko Juu Ya Kupendelewa Morocco Je ni Sahihi?


 Senegal ndio mabingwa wa awamu ya 35 ya michuano ya soka barani Afrika afcon yalioandaliwa nchini Morocco.

Hii ni baada ya kuwachabanga wenyeji Morocco bao moja kwa nunge kwenye fainali ya kihistoria iliyokuwa na matukio mengi yenye utata yaliochafua hadhi ya mashindano hayo katika ulimwengu wa soka.

Tukio kuu katika fainali hiyo litakalosalia katika kumbukumbu ya historia ya michuano hiyo ni katika dakika ya 98 pale Senegal walipotoka uwanjani na kususia mechi hiyo kwa muda wa dakika 17.

Chanzo kikiwa ni uamuzi wa refa Jacques Ndala aliyewatuza Morocco penalti baada ya kutumia uamuzi wa VAR. Malick Diouf wa Senegal alidaiwa kumchezea rafu mshambulaiji wa Morocco Brahim Diaz.

Kwa jadhba na ghadhabu, kocha wa Senegal Pape Thiew aliwaamrisha wachezaji wake kutoka kabisa uwanjani akilalamika kuwa wamedhulumiwa.

Mchezaji aliyebaki uwanjani ni Sadio Mane tu, nahodha wa Senegal aliyewashauri wenzake kurejea, na baada ya dakika 17 walirejea na kukubali kuendelea na mchezo.

Kwa bahati nzuri kwa Senegal, Brahim Diaz aliyefunga mabao 5 kwenye michuano hIiyo, aliipiga penalti hiyo iliyonyakwa na kipa Eduad Mendy wa Senegal. Hakufunga

Katika muda wa dakika 30 za ziada Senegal waliojikakamua walifunga bao dakika nne kipindi cha kwanza cha muda wa ziada ,mfungaji akiwa Pape Gueye.

Post a Comment

0 Comments