Simba SC kumkosa Mwalimu Mechi Tatu.


Mshambuliaji wa Simba Sc “Selemani Mwalimu” amefungiwa na Bodi ya Ligi kwa michezo Mitatu na Faini ya Shilingi Millioni (1,000,000)
‎Kwa kosa la kumpiga Kiwiko kwa makusudi mchezaji wa (Dodoma Jiji) “Andy Lobulka Bikoko”
‎Kwa maana hiyo Sele, atakosa michezo ifuatayo: 👇🏼
‎🆚 B19 March, 7 (CRDB CUP)
‎🆚 TRA United, March 14
‎🆚 Pamba Jiji, March 19
‎Klabu ya Simba pia Imetozwa Faini ya Shilingi millioni (5,000,000) kwa kosa la mashabiki wake kumrushia chupa za maji mchezaji wa (Dodoma Jiji) “William Edgar” wakati akitoka uwanjani.
‎Pamoja na mashabiki wao kuwarushia chupa watoa huduma ya Kwanza (Redcross) wakati wakitekeleza majukumu Yao.
‎Klabu ya (Dodoma Jiji) pia Imetozwa Faini ya Shilingi Millioni (5,000,000) kwa kosa la maofisa wake wa Huduma ya kwanza (Redcross) kuonekana mara kadhaa wakichelewa kwa makusudi pale walipotakiwa kufanya hivyo.

 

Post a Comment

0 Comments