Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, ambaye leo anatimiza
miaka 41, huenda anatarajiwa kususia mechi ya pili kwa Al-Nassr licha ya
kuchapisha picha yake akifanya mazoezi, na badala yake akaomba kuondoka katika
klabu hiyo ya ya Ligi Kuu ya Saudi Pro mnamo mwezi Juni. (ESPN)
Ikiwa Ronaldo
ataondoka Al-Nassr, kuna uwezekano mkubwa wa kurudi katika klabu yake ya kwanza
ya Sporting Lisbon. (Fichajes - kwa Kihispania)
Kiungo wa kati wa
Ureno Ruben Neves, 28, ambaye alihusishwa na uhamisho wa Januari kwenda
Manchester United miongoni mwa vilabu vingine, amesaini mkataba mpya katika
klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal hadi Juni 2029. (Fabrizio Romano)

0 Comments