JKT Tanzania Mambo Safi Ligi Kuu


 ‎Baada ya ushindi dhidi ya Mashujaa na kufikisha pointi 27 katika mechi 15 za Ligi Kuu, JKT Tanzania imebakiza ushindi tatu (pointi tisa) ili kufikia rekodi ya alama 36 ilizokusanya msimu uliopita katika mechi zote za msimu.

‎Tofauti na msimu uliopita ambapo baada ya mechi 15 walikuwa na pointi 19, safari hii JKT Tanzania tayari imefikisha pointi 27 na inaongoza msimamo, ikiwa imeongeza pointi nane zaidi kulinganisha na kipindi kama hiki msimu uliopita.

‎Katika msimu huu, JKT Tanzania imeshinda mechi sita baada ya michezo 15, wakati msimu uliopita ilikuwa imeshinda nne pekee katika idadi hiyo ya mechi. Hadi sasa imepoteza michezo miwili dhidi ya Simba na Dodoma Jiji, idadi inayolingana na vipigo ilivyokuwa navyo kufikia hatua hii msimu uliopita.

‎Kwa mwenendo huu, JKT Tanzania inaonekana kuwa kwenye kasi bora zaidi na ina nafasi kubwa ya kuvunja rekodi yake ya alama za msimu uliopita.

Post a Comment

0 Comments