Mwanzoni mwa msimu mashabiki wa Liverpool waligundua jambo kuhusu Liverpool. Lilihusu tabia ya kufunga magoli katika dakika za mwisho za mchezo.
Federico Chiesa alishangalia bao lake la dakika 88 dhidi ya Bournemouth siku ya ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu England. Kabla ya Mohamed Salah kufunga bao katika dakika za mwisho na kuweka matokeo 3:2.
Kijana Rio Ngumoha alifunga bao la ushindi katika dakika ya 100 huko St James' Park huku Newcastle ikishindwa 3-2.
Wiki moja baadaye Dominik Szoboszlai alifunga bao katika dakika ya 83 dhidi ya Arsenal, na wikendi iliyofuata Salah alifunga penalti dakika ya 95 dhidi ya Burnley - ushindi wa 1-0.

0 Comments